WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema wanafanya uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha za miradi kwenye mikoa mitatu ambayo ni Mbeya, Singida na Iringa na kwamba ikibainika kuna ubadhilifu fedha hizo wahusika watazitapika.
Fedha zitakazotapikwa ni zile za miradi ziliozotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) Sh Trilioni 1.3 kwa ajili ya kuinua Uchumi.
Bashungwa akifafanua amesema kwa upande wa jiji la Mbeya mapato nusu mwaka yameshuka pia kuna pos (Mashine za kieletroniki za kukusanya mapato), zaidi 72 zilizimwa kwa zaidi ya siku 100.
“Mheshimwa Rais, tupo tunachunguza ni kwa nini pos hizo zilizimwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato, tayari nimeshaunda tume na badae tuchukue hatua,” ameeleza Bashungwa na kuongeza.
“Pia kuna Halmasharui ya Geita Vijijini baada ya Mbunge Joseph Musukuma kutoa tuhuma kuna ubadhilifu katika halmashauri ile, nako pia nimeunda tume tunafanya uchunguzi kwa mujibu wa taratibu ili tusimuonee mtu.”
Bashungwa alisema kwa upande wa Singida kupitia Halmashauri Kuu ya Chama ya Mkoa, kulitokea changamoto upande wa Mkurugenzi na kwamba Tamisemi tumefanya uchunguzi kwa ajili ya kukuletea na kushauri nini kifanyike.”
Pia kwa upande wa Manispaa ya Iringa na maeneo mengine wanafanya tathmini kwa halmashauri zote fedha za maendeleo zilizoenda zimefanya kazi iliyokusudiwa na kwa usahihi.