Jackson Kikwete Asema Rais Samia Alipokea Wadhifa Huo Kipindi Kigumu




Chalinze. Rais mstaafu awamu ya nne, Jakaya Kikwete amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri wa Serikali na CCM, akisema kuwa alipokea wadhifa huo katika wakati mgumu baada ya kifo cha Hayati Rais John Magufuli.

Kikwete ameyasema hayo leo Februari 3 mjini Chalinze alipokua mgeni rasni wa sherehe za maadhimisho miaka 45 ya CCM yaliyofanyika ngazi ya mkoa viwanja vya Bwilingu.

Amesema kwa utaratibu, ilitakiwa Hayati Magufuli amalize muda wake na ndipo chama kitoe mgombea mwingine, lakini Rais Samia ameingia baada tu ya kifo cha Hayati Magufuli.

"Unajua ukigombea unatengeneza mipango yako mwenyewe kichwani, mimi niligombea mwaka 1995 kura hazikutosha, nilipokuja kugombea tena mwaka 2005.


“Nilijipanga kweli kweli nilikuwa na hakika nikipata uongozi wa nchi yetu nitafanya nini kwenye elimu, afya, barabara kwenye hiki na hiki, lakini mwenzetu Samia yeye amejikuta ghafla tu amekabidhiwa uongozi wa nchi.

"Lakini alichotushangaza wengi ni kupokea uongozi kwa kujiamini na kwa ujasiri mkubwa na kuendesha mambo vizuri, anaongoza Chama na Serikali na mambo yanakwenda vyema, matokeo yake tunayaona. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye, masikio ahambiwi sikia."

Awali Mwemyekiti CCM Bagamoyo, Abdulzahor Sharrif alimuomba Kikwete akawaombee kwa Rais Chalinze ipewe hadhi ya wilaya na kwamba kama kwa ngazi ya kiserikali michakato itakua inachukua muda basi waruhusiwe ianze kwa upande wa kichana (wilaya kichama).


Hata hivyo, Kikwete alilikataa ombi hilo hadharani na kuwata waende wenyewe chama kwa mwenyekiti Taifa wakamweleze ombi lao hilo.

"Hili la Ombi la Mwenyekiti wa Bagamoyo, mimi sifikishi msije kunidai bure, fikisheni wenyewe," alihitimisha kuhutubia
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad