Jamhuri yaomba Rufaa ya Sabaya itupwe



Arusha. Mawakili wa Serikali wameiomba Mahakama Kuu kanda ya Arusha kuitupa rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, waliohukumiwa kufungo cha miaka 30 jela kwa unyanyaji wa kutumia silaha kwa kuwa haina mashiko kisheria.

Mbele ya Jaji  Sedekia Kisanya, Wakili wa  Jamuhuri, Verediana Mlenza alidai leo Februari 18,2022, kuwa hoja iliyowasilishwa mahakamani kwamba hakimu alikosea kupokea kielelezo namba 4, 5 kwa kuwa vilikuwa vimepikwa  haina msingi wa kisheria na hakuna ushahidi unaopinga vielelezo hivyo tangu awali .

Alidai hoja hiyo hazijawahi kuibuliwa wakati vielelezo vilipowasilishwa mahakamani, hivyo mawakili kuibua hoja hiyo sasa si sahihi na pia hakuna mahali mawakili wakati wa ushikilizwaji wa kesi hiyo walionyesha polisi walipika hivyo vielelezo.

Akiendelea kutoa hoja ya kupinga rufaa hiyo, Wakili Mlenza ameeleza hoja nyingine waliyoilalamikia ni kwamba haikuwa sawa upande wa mashtaka kurekebisha hati ya mashtaka wakati walishafunga ushahidi, ni dhaifu kwa kuwa sheria iko wazi kwamba hati inaweza kubadilishwa muda wowote kabla ya hukumu kutolewa.

Jaji anayesikiliza rufaa hiyo, Sedekia Kisanya ameahirisha shauri hilo hadi Februari 21, 2022 ambapo wajibu rufaa wataendeea kujibu hoja.

Sabaya na wenzake wawili; Sylvesta Nyegu na Daniel Mbura  walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja Oktoba 15, mwaka jana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad