Wiki hii imekuwa ngumu sana kwa wamiliki wa mtandao wa Facebook mara baada ya jana kutangazwa kupoteza kiasi cha ($237 BILLION) ya hisa zake ndani ya siku moja, ikiwa ni kiwango kikubwa kuwahi kutokea katika historia ya kampuni hiyo ambayo sasa inatambulika kama Meta.
Fedha hizo zaidi ya TSh. Trilioni 547.9 zimepelekea kuathiri utajiri wa CEO Mark Zuckerberg ambapo amepoteza kiasi cha ($29.7 million) zaidi ya TSh. Trilioni 67 kwenye utajiri wake, Jumatano alikuwa nafasi ya 7 kwenye orodha ya matajiri duniani akiwa na kiasi cha ($113 billion) zaidi ya TSh. Trilioni 261 lakini jana Alhamis amejikuta nafasi ya 12 akiwa na kiasi cha ($83.4 billion) zaidi ya TSh. Trilioni 192.
Si hivyo tu, Facebook pia ilishuhudia ikianguka upande wa watumiaji wa siku (Daily Active Users) ambapo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 18, ikipoteza watumiaji takribani 500,000 kwenye miezi mitatu ya mwisho kwa mwaka 2021. Ripoti za kampuni ya Meta zinaonesha Facebook imeanguka toka watumiaji wa siku BILIONI 1.93 hadi BILIONI 1.929