Kimbunga Batsirai Chatabiriwa Kutua Tanzania



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Batsirai katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi.

TMA imesema inaendelea kufuatilia kimbunga hicho tangu kilipojitokeza katika bahari ya Hindi tarehe 27/01/2022 na kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa kimbunga Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania.

Hata hivyo uwepo wa kimbunga Batsirai baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua; vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.


 
Maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa kutokana na uwepo wa kimbunga hicho baharini kati ya tarehe 04 hadi 08/02/2022 ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa. Hata hivyo mvua za Msimu zinaendelea katika maeneo mengine yanayopata mvua hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad