Kimeumana! Darassa, Jux Wamvaa Harmonize



WASANII maarufu wa Bongo Fleva, Juma Jux na Sheriff Thabeet ‘Darasa’ wamemvaa msanii mwenzao ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lebo ya Konde Gang, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ baada ya majina yao kuonekana kwenye orodha ya wasanii ambao watatumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival, Machi 5, mwaka huu, kwa mujibu wao wamenadai kwamba hawakupewa taarifa.

Jux ameandika ni vyema uongozi wa Harmonize ungewasiliana na menejimenti yake kabla ya kuweka tangazo hilo mtandaoni, amemtaka kulifuta haraka kwa kuwa yeye Binafsi alimtafuta Konde Boy na kumuelezea hatua alizozipitia kwenye makubaliano kuwa sio sahihi lakini hawakuchukulia Serious Ishu hiyo.

Jux amesema kuwa, “Ni Kweli #Harmonize aliwahi Kumtafuta na kumuelezea kuhusu hili Tamasha, na baada ya hapo hawakuongea tena lolote kuhusu malipo na litafanyikaje na ratiba yake ipoje, ila walikubalina vitu vikiwa tayari waambiane kwa ajili ya mikataba, leo aliamka na kukuta tangazo limewekwa tayari kuwa atakuwepo kwenye shoo.

African Boy ameongeza kuwa baada ya kuliona Tangazo mtandaoni linasambaa sana likiwa na jina lake, alitafuta Uongozi wa Konde Music lakini hakupewa majibu yanayoridhisha, kisha alimtafuta yeye mwenyewe #Harmonize na kumuelezea na hata baada ya hapo Tangazo hakulitoa na aliliacha liendelee kuwepo kwenye page.


 
Aidha, Jux ameongeza pia kwamba kuwa kitendo hiko sio sawa kwenye muziki na biashara yake, lakini pia huwa ana mawasiliano binafsi na Harmonize hivyo haelewi Ushikaji Unapitiliza au kumchukulia Poa au Kama Dharau kwa upande wake.

Kwa upande wake, Darassa naye ameshusha malalamiko yake akidai wasanii wanapenda kupeana support lakini ni vyema kama Harmonize angewapa taarifa kabla ya kuwabandika kwenye tangazo.




Baada ya sekeseke hilo, Harmonize ameamua kui-delete poster hiyo na kuyafuta majina ya Jux na Darassa kwenye bango lenye orodha ya wasanii ambao wametajwa kutumbuiza kwenye tamasha lake hilo kisha kuweka bango jipya ambalo ambalo majina ya wakali hao yameondolewa bila kusema iwapo alikosea ama alikuwa amewasiliana nao kabla.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad