Ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ilimuweka matatani aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr Hamis Kigwangalla baada ya kubainisha uwepo wa viashiria vya ubadhirifu wa fedha kutokana na kanuni mbalimbalki kukiukwa.
Akiwa Waziri, Kigwangalla alianzisha tamasha la urithi pamoja na uhamasishaji wa kupanda Mlima Kilimanjaro, lengo likiwa ni kuhamasisha utalii nchini. Ikiwa muda sasa umepita tangu tuhuma hizo zitolewe.
Dr Kigwangalla amesimama leo Feb 17 2022 bungeni wakati bunge likipokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021, Kigwangalla alipata nafasi ya kuchangia ambapo alitaka kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja za CAG ambazo zilimtuhumu ambapo hakupata nafasi ya kueleza baada ya Spika Dr. Tulia kumtaka kutumia njia sahihi kukanusaha taarifa hizo ndipo alipokutana na wanahabari na kukanusha taarifa hizo.
Tazama Video