Kirusi kipya cha HIV kimegundulika Uholanzi ambapo Wataalamu wanasema ni hatari zaidi kuliko kirusi kilichozoeleka siku zote kwani kirusi hiki kipya kinamshambulia Mtu kwa haraka mara mbili zaidi ya kirusi cha siku zote.
Kirusi hiki kipya kilichopewa jina la 'VB Variant' tayari kimewapata Watu 109 wengi wao wakiwa ni kutoka Uholanzi na inaelewa kwamba kinaharibu na kushambulia kinga ya mwili mara mbili ya kirusi kilichozoeleka na hadi sasa haijapatikana dawa yake wala chanjo ya kupambana nacho.