Kisa Michezo Michafu ya Wachezaji Yanga..Kocha NABI Aibuka na Hili Jipya



KUFUATIA wachezaji wa Yanga, Dickson Job na Djuma Shabani, kusimamishwa kucheza mechi za ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na makosa waliyofanya katika michezo iliyopita, kocha wa timu hiyo, Nasraddine Nabi, ameibuka na kuwaonya kutorudia vitendo hivyo la sivyo atachukua mshahara wote.
Djuma alisimamishwa na Bodi ya Ligi kucheza mechi tatu baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania, Yahaya Mbegu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, ambapo Yanga ilishinda kwa bao 1-0, huku Job akipewa adhabu baada ya kumchezea rafu, Richardson Ngodya wa Mbeya City hivyo na yeye kusimamishwa michezo mitatu.

Chanzo chetu kutoka Yanga kimeliambia Championi kuwa, pamoja na Bodi ya Ligi kutoa maamuzi yake, Nabi naye katoa onyo kali kwa nyota hao ambapo amewataka wachezaji wote wa Yanga kuepuka makosa ya kizembe ambayo yanaweza kuigharimu timu kwa kukosa huduma zao uwanjani.

“Kocha ameitisha kikao mara baada ya Djuma na Job kupewa adhabu ya kukosa mechi tatu, aliwaambia mara nyingine ataondoka na mshahara wa mchezaji atakayeonekana kusimamishwa baada ya kufanya kosa la kizembe.

“Kocha amewaambia wachezaji kujichunga sana katika kudhibiti hasira kwani endapo hawatakuwa makini basi wanaweza kujikuta takribani kila mechi kuna mchezaji anasimamishwa kwani kutokana na mwenendo wa timu kwa sasa wapinzani wanahakikisha wanawachokonoa ili wapate adhabu ambayo itawapunguza kasi,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara alisema: “Samahani niko hospitali, nitakupigia.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad