MZEE wa spidi 120, Tuisila Kisinda ambaye kwa sasa yupo ndani ya RS Berkane amesema kuwa anaweza kuja kucheza Tanzania tena ikiwa Yanga watahitaji huduma yake.
Kisinda alikuwa anacheza Yanga alijiunga na RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu wa 2021/22 na jana alikuwa katika kikosi cha kwanza kilichoshinda mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya makundi ambapo Simba ipo kundi D.
Kisinda amesema:”Naongea tu Yanga ni nyumbani kama bosi ananitaka ninarudi kucheza fresh, tutaongea tu fresh.
“Kwenye mpira hapa tunacheza na Tanzania tunaweza kucheza kwenye mpira fresh tu kila kitu kinawezekana,”.