JURGEN Klopp amekiri kuwa hakuna aliyetarajia kuwa Mo Salah atakuwa gwiji wa kufunga mabao Liverpool haraka namna hiyo kufuatia Mmisri huyo kufunga bao lake la 150 juzi kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Norwich.
Salah alionekana atakuwa wa kawaida tu aliposajiliwa na Liverpool kutokea Roma kwa pauni mil 36 mwaka 2017 kutokana na kucheza kawaida alipokuwa na Chelsea hapo awali.
Hata hivyo, alifunga katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Watford na tangu hapo hajaacha kufunga. Sasa amefikisha mabao 150 katika mechi 233, na ameweka rekodi ya kuwa na uwiano bora zaidi wa mabao ukilinganisha na mechi alizocheza, kuliko mchezaji yeyote wa Liverpool kihistoria ambaye ameifungia klabu hiyo mabao zaidi ya 30.
Hii maana yake ni kwamba amefikisha idadi ya mabao 150 kwa haraka zaidi, yaani katika mechi chache zaidi.
“Bao lake la kwanza pale Watford pengine ndilo lilikuwa rahisi zaidi. Alifunga mabao mengine 149 ndani ya kipindi kifupi sana,” alisema Klopp.
“Siwezi kukumbuka mabao yake yote lakini nayakumbuka mengi na kulikuwa na mabao mengine mazuri zaidi. Dhidi ya Chelsea, akifunga kutoka kwenye kona, alipofunga baada ya kukokota mpira dhidi ya Manchester City, dhidi ya United kwa pasi ya Alisson. Na leo (juzi) lilikuwa bao zuri kusema ukweli.”
Salah sasa amekuwa mmoja wa wachezaji 10 tu katika histori