Kocha Misri Aomba Fainali Kusogezwa Mbele



KOCHA msaidizi wa Misri Diaa al-Sayed anataka fainali yao ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal ichezwe Jumatatu badala ya Jumapili ili wapate siku ya ziada ya kupumzika.

 

Mafarao waliwashinda wenyeji Cameroon siku ya Alhamisi kwa mikwaju ya penalti, ukiwa ni ushindi wao wa tatu mfululizo.

Senegal, ambao wameshinda michezo zao zote ndani ya dakika 90, walishinda Burkina Faso 3-1 Jumatano.

“Naomba CAF fainali ichezwe Jumatatu,” Senegal wana siku moja ya ziada ya kupumzika” alisema Al-Sayed.

 

Al-Sayed alikuwa akizungumza na vyombo vya habari kwa sababu kocha wa Misri Carlos Queiroz alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati wa mechi.

 

Mechi ya kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu kati ya Cameroon na Burkina Faso ulipaswa kuwa Jumapili pia, lakini sasa itachezwa Jumamosi tarehe ya fainali iksogezwa itachelewesha wachezaji kurejea kwenye vilabu vyao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad