Kotinyo "Malalamiko ya Haji Manara Yameegemea Kwenye Timu Mbili tu, Hayana Maslai Kwa Taifa na Ligi"


Ukimsikiliza Haji Manara, utagundua maelezo yake yote yamelala kwenye timu mbili tu [Simba na Yanga] na hapo ndipo huwa naamua kupuuza malalamiko au kumbukizi kama hizi.

Tukiwa wakweli, sio Simba na Yanga peke yake ambazo zinanufaika au kuathirika na baadhi ya makosa ya waamuzi. Unapokuja mbele na hoja zako za timu mbili pekee huwezi kusema ni kwa ajili ya manufaa ya taifa wala timu ya taifa.

Ukiachana na matatizo ya waamuzi, hivi vilabu ndio vinaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi wa kigeni, hivi vilabu vingine ndio tuna vitegemea kuzalisha wachezaji wenye ubora kwa ajili ya timu ya taifa.

Simba wamenufaika lakini Yanga wamenufaika pia na makosa ya waamuzi, vilabu vyote hivi kwa pamoja vimenufaika dhidi ya vilabu vingine ila sio walipokutana wao kwa wao. Kwa hiyo kutoka mbele kwa kuzifanya Simba na Yanga ndio kilelezo cha kuathirika au kunufaika kwa baadhi ya maamuzi hautendei haki mfumo mzima wa Ligi.

Lakini kama kuna matukio ya maamuzi tata yanatokea kwenye mechi ya Polisi Tanzania dhidi ya Namungo na timu moja wapo ikanufaika halafu hausemi, basi usiseme unaipigania haki ya Ligi.

Ukweli ni kwamba, waathirika wakubwa wa maamuzi si Simba na Yanga. Vilabu vingine ndio havipati faida ya vinapocheza na timu hizi mbili lakini hata vikilalamika nani anasikiliza?

- Nicasius Agandwa [@kotinyotz]
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad