Kubenea: Bila Rais Samia Magazeti Yangu Yasingerudi



MKUREUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea, amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kufungua ukurasa mpya na vyombo hivyo vya habari baada ya kuyafungulia magazeti yake ya Mwanahalisi na Mseto huku akisisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali.

Kubenea amesema hayo leo Alhamisi, Februari 10, 2022, wakati akizungumza mara baada ya kupokea leseni za magazeti yake hayo zilizotolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

“Ni muhimu sana viongozi kusikiliza, hakuna aliyekamilika… Tukuahidi kwamba tutakwenda kufanya kazi kwa weledi, kwa kufuata misingi ya uandishi wa habari, sheria za nchi, usalama wetu na kuangalia zaidi maslahi ya nchi yetu.

“Nikushukuru Waziri Nape kwa hatua kubwa kufungua ukurasa mpya kwa kutupa leseni, magazeti haya yalimaliza adhabu miaka miwili bado yalishinda kesi mahakamani lakini hayakurudi, tunamshukuru Rais Samia kwani bila yeye yasingerudi


 
“Tumepata leseni, lakini inawezekana kabisa hayo magazeti usiyakute mtaani. Hali ya uchumi ni mbaya sana. Magazeti yapo ambayo hayakufungiwa, yalijifunga yenyewe… Serikali iangalie namna ambavyo inaweza ikatoa ruzuku kwa vyombo vya habari binafsi.

“Ni muhimu sana viongozi kusikiliza, hakuna aliyekamilika… Tukuahidi kwamba tutakwenda kufanya kazi kwa weledi, kwa kufuata misingi ya uandishi wa habari, sheria za nchi, usalama wetu na kuangalia zaidi maslahi ya nchi yetu. Mhe. Waziri [Nape Nnauye] kwa niaba ya wenzangu nikushukuru sana kwa kufungua ukurasa huu mpya na vyombo vya habari nchini,” amesema Kubenea.

Magazeti mengine yaliyokuwa yqamefungiwa na yamefunguliwa leo ni Tanzania Daima na Mawio ambayo yote yalikuwa kifungoni kwa miaka kadhaa kwa madai ya kukiuka sheria, kanuni na miiko ya uandishi wa habari.
 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad