Oscar Ikinya (43) Mfanyakazi wa zamani wa Bank ambaye alinusurika kwenye mlipuko wa bomu 1998 huko Nairobi Kenya ambaye anaamini anaugua Trimethylaminuria (TMAU) unaojulikana kama ugonjwa wa samaki.
Kwa zaidi ya miaka 20, amekuwa akiishi peke yake kwa sababu ya harufu yake ya mwili, alihamia eneo tofauti nchini Kenya na kwa miaka saba akiishe peke yake hana mke wala mtoto.
Healthy Nation ya Nchini Kenya ilithibitisha kuwa Oscar ana hilo tatizo la TMAU (trimethylaminuria) ambao ni ugonjwa nadra husababisha mtu kuwa na harufu mbaya, ya samaki ambayo hutolewa kwa jasho, mkojo, pumzi, na maji ya uzazi.
Trimethylamine ni harufu kali inayotoka kwa samaki waliooza hii ndio maana ukaitwa ugonjwa wa harufu ya samaki.