Kusah "Ruby Anaumia Kuona Nafanikiwa Nikiwa na Aunty, Namshauri Atengeneze Marafiki Kuliko Maadui"



Kupitia waves za Empire ya EFM, @_kusah_ amemtaka @iamrubyafrica kupambania alicho nacho (kipaji cha muziki) kwa maana ni kikubwa zaidi ya anacho kifanya saa hii cha kumuandama mitandaoni, na pia anamsihi atengeneze marafiki wengi kuliko maadui maana haya maisha ni mafupi sana.

Kusah ameendelea kuapa kuwa anatokea Tanga vijijini lakini Mama yake hata siku moja hajawahi kumshauri aende kwa waganga,hata kumtuma kwenda kutafuta dawa ya kichwa, inamuumiza kuona anahusishwa kwenye mambo ambayo si ya kweli.

Anachohisi kwa Rubby ni kuona baada ya kuachana anaumia kuona Kusah anafanikiwa, Kusah Amedai hakuna jipya kwa Ruby atalosema yeye akaumia zaidi ya kuona anamuhusisha hadi mama yake mzazi, maana ashawahi andika bango refu,akimwita Marioo,alimkuta analala studio,hana hela, ila kwasasa Kusah ni mkubwa kuliko yeye, kamzidi hadi subscribers, hivyo hawezi tenga muda wake kuanza kujibizana nae.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad