Kwa Wale wa Matangazo, Kutangaza Kwenye Page ya Instagram ya Christiano Ronaldo ni Shilingi Bilioni 4 Kwa Post Moja


Mitandao mbalimbali Uingereza kama Daily Mail na flipboard imeripoti kuwa kwa sasa Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo analipwa Euro milioni 1.7 ambayo ni Tsh. 🇹🇿 Bilioni 4+ tsh. 🇰🇪 milioni 220+ kwa post moja ya tangazo la kibiashara atakalo-post kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Cristiano Ronaldo ambaye juzi kati amefikisha followers milioni 400 Instagram baada ya ongezeko la followers milioni 124 ndani ya miezi 10 iliyopita, kwa sasa ndiye kiumbe anaeshikilia rekodi ya kuwa na followers wengi zaidi kwenye Instagram na pia kiumbe wa kwanza kufikisha followers milioni 400.

Mwezi September mwaka 2021 wakati Rinaldo hajafikisha followers alionao sasa alikuwa analipwa Euro 1,019,100 kwa post moja ya Instagram ambayo ni sawa na pesa za kitanzania 🇹🇿 Bilioni 2. 693, Ksh. 🇰🇪 milioni 132.3
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad