TMA yatoa angalizo mvua kubwa na upepo mkali

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kwa wananchi juu ya hali ya hewa katika siku kadhaa zijazo.
JUMAPILI 06-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Ruvuma Lindi na Mtwara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMATATU 07-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma Lindi na Mtwara.

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMANNE 08-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMATANO 09-02-2022
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

Utabiri huu umetolewa,
Na, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad