Dodoma. Wabunge wanafanya uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania atakayechukua nafasi nafasi iliyoachwa na Job Ndugai aliyejihuzulu nafasi hiyo Januari 6, 2022.
Uchaguzi huo unaofanyika leo Jumanne Februari Mosi 2022 jijini Dodoma unaongozwa na Mwenyekiti wa uchaguzi, Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi ambaye amepitishwa na wabunge kuongoza uchaguzi huo.
lukuvi pic
Mbunge wa Ismani, William Lukuvi akizungumza bungeni alipokuwa akiongoza kikao cha kumchaguwa Spika wa Bunge, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Akizungumza bungeni kabla ya kuanza uchaguzi huo, Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi amesema wagombea wa kiti hicho wapo tisa.
Amewataja wagombea hao kuwa ni pamoja na Naibu Spika, Dk Tulia Akson anayeiwakilisha CCM, Abdullah Mohamed Said (NRA), Aivan Maganza (TLP), Daivd Mwaijojele (CCK) na Georges Busungu (ADA-TADEA).
Wengine ni pamoja na Kunje Ngombale Mwiru (SAU), Maimuma Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP) na Saidoun Abrahamu Khatibu ambao wote.