Lukaku Aipelekea Chelsea Fainali Kombe la Dunia



Mshambuliaji cha Chelsea, Romelu Lukaku amefanikiwa kufunga bao dakika ya 32 na kuifanya timu yake iibuke na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Saudi Arabia na kuisaidia timu yake kutinga fainali ya kombe la Dunia la Vilabu.
Hii ni mara ya kwanza michezo ya fainali za Kombe la Dunia la Vilabu kufanyika kwenye Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu huku ikishuhudiwa Chelsea ikipewa wakati mgumu na mabingwa wa Saudia, Al Hilal kwenye dimba la Mohamed bin Zayed, Abu Dhabi nchini humo.

Licha ya Chelsea kumkosa kocha wake Mkuu, Thomas Tuchel aliyekuwa karantini lakini haikuwazuia matajiri hao wa jiji la London kupata ushindi huo mwembamba mbele ya matajiri wa Saudia.

Al Hilal ilikuwa ikiongozwa na nyota wa zamani wa Manchester United, Mnaigeria Odion Ighalo na Moussa Marega raia wa Mali ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea FC Porto ya Ureno kwenye Michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Kwa upande wa benchi la Ufundi, Leonardo Jadim kocha wa zamani wa AS Monaco aliyewapa ubingwa wa Ligue 1 msimu wa 2017 ndiye aliyekuwa anasaka rekodi ya kutinga fainali ya kombe hilo lakini haikuwezekana.


Sasa Chelsea itacheza fainali hiyo hiyo dhidi ya wababe wa Amerika kusini, klabu ya Palmeiras ya Brazil Februari 12, 2022 kwenye dimba la Mohamed bin Zayed, Abu Dhabi ambapo itakuwa ni fainali ya pili kwa Chelsea baada ya miaka 9 kupita walivyofungwa na Corinthias ya Nchini Brazili 1-0 Yokohama nchini Japan hivyo ni shauku kubwa kwa Tajiri wa klabu ya Chelsea, Roman Abromovic kushuhudia Chelsea ikibeba Ubingwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad