Maajabu ya Maporomoko ya Maji Yanayofanana na Damu




Hebu vuta picha, mto unatiririsha maji na kuna sehemu kuna maporomoko ambapo maji yanadondoka kutoka juu mpaka chini lakini tofauti na maji ya kawaida, maji haya yana rangi kama damu! Ni tukio la kustaajabisha si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako, kwenye Bara la Antarctica, kuna sehemu inaitwa Victoria ambapo kuna maporomoko maarufu yaliyopewa jina la ‘blood falls’ au kwa Kiswahili maporomoko ya damu, ambapo maji yanandondoka umbali unaoweza kufananishwana urefu wa ghorofa tano, yakiwa na rangi kama damu na kuingia kwenye Ziwa Bonney.

Wapo watu wanaoyahusisha maporomoko hayo na nguvu za giza, wengine wanalitaja eneo hilo kuwa takatifu, wengine wanasema ni eneo ambalo dunia inatokwa na damu kutokana na maasi ya wanadamu, ilimradi kila mmoja anasema lake.

Maporomoko haya, yaligunduliwa na mwanasayansi wa Australia, Griffith Taylor mwaka 1911 akiwa kwenye ziara ya utafiti wa theluji ya eneo hilo na kama heshima kwake, eneo hilo baadaye lilikuja kupea jina la Taylor Glacier.


 
Nini kinasababisha maji yawe na rangi kama damu?Ni kweli kuna nguvu za giza? Kiasili, eneo la Taylor Glacier kuna hali kama ya jangwa na theluji inayorundikana eneo hilo, hukaa juu ya jangwa na kuyeyuka kipindi cha joto. Ardhi ya eneo hilo inatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha chumvi, madini ya sulphate na chembechembe za chuma, ferrous ions.

Kwa kuwa eneo hili lipo kwenye ncha ya dunia, mgandamizo wake wa hewa huwa ni mdogo kwa hiyo chumvi na madini hayo, huwa hayayeyuki vizuri kwa sababu ya mgandamizo wa hewa. Joto linapoongezeka, maji huyeyuka na kuanza kutiririka kuelekea kwenye maeneo ambayo mgandamizo wake wa hewa huwa ni sawa na sehemu nyingine za dunia, au kwa kitaalamu atmospheric pressure.


Maji hayo yanapofika kwenye maeneo yenye hali ya hewa ya kawaida, chumvi huyeyuka sambamba na yale madini mengine na kama inavyofahamika, chumvi inapokutana na madini ya chuma, husababisha kutu ambayo rangi yake inakuwa na wekundu, kwa hiyo mchanganyiko huo huyafanya maji yote kuwa na rangi nyekundu na huendelea kutiririka mpaka kwenye maporomo hayo.


Na Aziz Hashim

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad