Inaelezwa kuwa Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika mashariki na kati
Uongozi wa Hospitali hiyo umesema Upasuaji huo maalum umefanywa kwa mwanaume mwenye miaka kati ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari kushiriki tendo la ndoa
Tatizo hilo ambalo kitaalamu linaitwa Erectile dysfunction (ED) inaelezwa kuwa limemsumbua kwa miaka kadhaa
Wataalamu wanasema Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo
Kwa Mujibu wa wataalamu hao wanasema upandikazaji unahusisha kuweka kifaa maalumu (Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhitajika kutumia dawa nyingine
Huu ni Upasuaji wa kwanza kufanyika katika ukanda huu