MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo Jumanne tarehe 8 Februari 2022, imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lengo ni ili kumwezesha Makonda kupata taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari mwandamizi, Saed Kubenea.
Kubenea amefungua maombi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Makonda mwenyewe.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Aron Lyamuya ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2 Machi 2022.
Ametoa uamuzi huo baada ya mawakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama kutoa samasi ya kumtangaza kwani jitihada za kumpata Makonda ili kupatiwa wito wa kufika mahakamani kugonga mwamba.