"Kwa mliouliza kama nitakwenda Tanzania kumzika Dr. Mwele, hapana sitokwenda nitaishia hapa Geneva. Nitaagana na mama yangu hapa Geneva na ntahakikisha kapanda kwenye ndege kwanza ndo ntarudi marekani.
Sitokuja Tanzania kumzika mama yangu for obvious reasons. Kipindi cha Magu nilifunguliwa kesi ya uhaini, hiyo kesi haijafutwa hadi sasa. Na hiyo kesi haina dhamana. Yes mama Samia amefuta makesi yote ya wapinzani yaliyofunguliwa kipindi cha Magu ila yangu bado haijafutwa na kuna arrest warrant ya kesi hiyo. Mbali na hapo bado kuna watu wapo kwenye system kama Sirro ambao niliwapa ukweli mchungu kipindi cha Magu, so of course iwe isiwe lazma watataka kunikomesha.
Sasa haitokuwa fair kwa mama yangu nifike Dar then attention yooote iwe Mange namakesi yake. Badala ndugu na familia wahangaike na msiba waanze kuhangaika na mambo ya ziada, huku msiba huku mambo ya Mange, hapana she deserves a better farewell that that. Hakuwa mtu wa drama sio sawa kuleta drama kwenye msiba wake…
Siku nikishuka bongo kwa mara ya kwanza hata wanangu siji nao, ntashuka nimevaa combat na buti tayari kupambana vita ya kesi zangu. Yani ntakuja kwa ajili ya ku-clear kesi zangu tu and nothing else.
Kuna some government officials wameniambia nije tu everything is okay, hii ni serikali mpya na hayo mambo yameshapita Ila I can’t take that risk kwenye msiba wa mamangu. Staki kutia doa msiba wa mama yangu kwa mambo yangu.
Inabidi niwe na subra kidogo kina Sirro wastaafu kwanza….
Ahsanteni sana kwa pole zenu. Ahsante sana kwa wooote mnaoendelea kunicheki naendeleaje. Mapenzi mnayoyaonyesha kwangu kwenye kipindi hiki kigumu yananifariji sana"Mange Kimambi
MANGE TUNAKUSUBIRI HATA KAMA UKIFA
ReplyDelete