Mastaa Yanga Wazuiwa Kula Burger, Pizza



KATIKA kuhakikisha wachezaji wake wanaepukana na majeraha ya mara kwa mara, Daktari wa Viungo waYanga,
MtunisiaYoussefAmmar amewapiga stop mastaa wa timu hiyo kutumia vyakula aina ya Burger na Pizza.


Hiyo ni katika kuhakikisha wanapunguza ongezeko la wachezaji wenye majeraha katika kikosi chao hicho ambacho kimepiga kambi hukoAvic Town, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.


Daktari huyo hivi sasa anawapambania nyota wake watatu warejee uwanjani ambao aliwapeleka nchini Tunisia kwa ajili yakufanyiwa upasuaji hivi karibuni kutokana na kuwa matatizo ya goti.

 

Wachezaji hao waliofanyiwa upasuaji ni Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Mburkinabe,Yacouba
Songne.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ammar alisema kuwa vyakula vya aina hiyo ya Burger na Pizza chanzo cha
wachezaji kupata majeraha yasiyotegemewa katika timu.

 

Ammar alisema kuwa tayari amewataarifu wachezaji kula vyakula vinavyohitajika ikiwemo ‘sea food’ili kuzuia majeraha yanayoepukika katika timu.


“Hili la ubovu wa viwanja lipo wazi kabisa, ndiyo chanzo cha wachezaji kupata majeraha kama vile magoti na enka ambalo kuepukika ni ngumu kutokana na miundombinu ya viwanja vya hapa nchini.


“Lakini lipo hili la vyakula, linaweza kuepukika kabisa kwa wachezaji kufahamu madhara watakayopata kutokana na vyakula ambavyo wanavyotakiwa kula katika maisha yao binafsi ya nyumbani tofauti na kambini ambako ni ngumu
kupikwa.


“Hivyo wachezaji hawatakiwi kula vyakula vya aina ya Burger na Pizza kwa faida yao na timu, kwani wanapokosekana katika mechi kutokana na tatizo la majeraha wanaidhohofisha timu,” alisemaAmmar

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad