Matibabu ya Prof Jay: Serikali, Chadema ‘wachuana’



WAKATI hali ya kiafya ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, mkoani Morogoro, Joseph Haule maarufu ‘Profesa Jay’ haijaimarika, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Serikali ni kama vile wanachuana kugharimia matibabu ya mwanasiasa huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wadadisi wa mambo ya siasa, wanafananisha mchuano huo kama uliotokea wakati Mbunge wa Iringa, Peter Msigwa (Chadema), alipogombaniwa kulipiwa faini kati ya Serikali na Chadema.

Msigwa na wabunge wenzake wanane, akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji walihukumiwa kwenda jela miezi mitano au kulipa faini ambayo kwa ujumla wake, ilikuwa Sh milioni 350.

Chadema iliitisha harambee na kuchangisha fedha hizo, ili kulipia wabunge wake, lakini Rais John Magufuli wakati ule alitangaza kumlipia Msigwa Sh milioni 40, huku Chadema ikijigamba kumlipia Mbunge huyo.

Profesa Jay ambaye pia ni msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, kwa takribani wiki tatu sasa, amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hali yake imeripotiwa kutoridhisha.

Gharama zake za matibabu, zimekadiriwa kufikia Sh milioni 20 ambazo familia yake iliweka wazi, kwamba haina kiwango hicho cha fedha.

Mwanahalisi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad