Mazishi ya Sonso yaisimamisha Tandale




Baadhi ya watu walijitokeza kwenye mazishi ya beki wao wa zamani Ally Mtoni 'Sonso'
Umati wa watu wanaokadiriwa kuwa maelfu umeshiriki mazishi wa aliyekuwa beki wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni 'Sonso'.

Watu wa rika mbalimbali wakiwemo 'watu wa mpira' wamejitokeza kwa wingi katika kukamilisha safari ya beki huyo aliyewahi pia kuzitumikia klabu za Kagera Sugar,Yanga na Lipuli ya Iringa.



Hata hivyo klabu za Namungo ya Lindi licha ya Sonso kutoichezea ilifika kushiriki mazishi hayo wakiungana na wenzao wa Ruvu na Yanga.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika Magomeni jijini Dar es Salaam umati mkubwa ulishiriki kuanzia nyumbani kwa wazazi wake mpaka makaburini.


 
Wakati mwili wa marehemu ukipelekwa makaburini umati wa watu ulilazimisha barabara ya Mtogole kufungwa kwa muda kupisha mazishi hayo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.



Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Mhandisi Hersi Said akizungumza kwenye mazishi ya beki wao wa zamani Ally Mtoni 'Sonso'
Watu hao walikuwa wkaigombania kubeba mwili wa beki huyo kabla ya kupelekwa makaburini ikiwa ni ishara kwamba kifo chake kimewagusa wengi.

Viongozi mbalimbali wa soka wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallece Karia walishiriki mazishi hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad