Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote.
Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.
Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.
Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.