Gloria Kibira (38) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto cha Kabwe, Kata ya Iyela jijini Mbeya amekutwa amenyongwa kwenye nyumba yake ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea tukio hilo akisema Mwili wa Marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba, Kagera kwa maziko. Watu wawili wanahojiwa kubaini chanzo cha mauaji