Mbowe, Wenzake Wanyimwa Chakula Miezi 5



KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania-Chadema, Freeman Mbowe ameibuka malalamiko mahakamani ya kunyimwa chakula kwa zaidi ya miezi mitano kila wanapokwenda kusikiliza kesi yao ya ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe kwa niaba ya wenzake watatu, amedai hayo leo Jumatatu, tarehe 14 Februari 2022, Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

“Sisi watuhumiwa tumenyiwma haki ya kula zaidi ya miezi mitano, tulipokuja kwenye mahakama yako, tumekosa haki ya kula kwa miezi mitano. Mheshimiwa jaji mnapokuwa mnaahirisha kesi kupata chakula cha mchana, sisi tumekuwa tukikosa chakula hata soda, sasa tunataka kujua kuna utaribu wa hivyo au Jeshi la Magereza kutupatia chakula au familia zetu kama wanavyotupatia,” amedai Mbowe

Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema, tulikuwa hatuli siku zote, mwanzoni tuliambiwa kama ni kula mchukue chakula kutoka gerezani mje nacho mahakani, sisi tuaishi jela hatuna friji kuhifahdi chakula, kwa hiyo tuletewe chakula Jumamosi tuhifadhi tukaona tutakula sumu. Tunaenda kukesha katika magereza bila chakula chochote hata soda hatupati.



Mara baada ya Mbowe kutoa malalamiko hayo, Jaji Tiganga akawauliza mawakili wa utetezi, “mmekuwa mkitoa uwakilishi gani mahakamani kama wateja wenu wanatuambia hawajala kwa miezi mitano? Nyie mko hapa mlikuwa mnawakilisha, hamkumuona kama ni haki ya wateja wenu?”

Baada ya Jaji Joachim Tiganga, kuhoji hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala akasimama kujibu akisema “tulifahamu ni tatizo awali, tukawasiliana na liaison officer wa magereza, akatuahidi atashughulikia.”

Jaji Tiganga ameahirisha kwa muda kesi hii na kuwaita mawakili wa pande zote mbili kujadiliana kuhusu suala hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad