"Mheshimiwa kufunga teknolojia ya VAR ni 346M kwa kiwanja kimoja ukizidisha kwa viwanja 10 utapata 3.46B, gharama za uendeshaji kwa mchezo mmoja inakadiriwa kuwa kati 10m mpaka 14m ukizidisha mara michezo ya ligi nzima unapata gharama yake.
Na tukumbuke tu VAR inatumika kwa matukio tu, kwahiyo kwa mchezo ambao hautokua na tukio la kuhitaji VAR tutakula hasara ya uendeshaji kwa mchezo husika.
Mheshimiwa pia umegusia nyasi bandia kwa viwanja..nadhani hili ndo la msingi kwasasa, achana na VAR ni anasa kulinganisha na uwanja ambalo ndio hitaji la msingi. Pesa ya VAR ongezea kwenye nyasi bandia, tukimaliza viwanja turudi kwenye taa za viwanjani ili tuondoe mechi za saa 8 mchana ambazo kuna baadhi ya timu hazipitii hii shida.
Asante." George Job