Mshambuliaji wa klabu ya Simba zamani Yanga Bernard Morrison ameanza tena kuteka vichwa vya habari kutokana na taarifa za vimbweka vyake anavyofanya kambini mitaa ya Msimbazi kuanza kuvuja.
Taarifa zinasema kuwa baadhi ya viongozi wamemtupia maneno na lawama kuwa anacheza chini ya kiwango makusudi siku za hivi karibuni na kubainika kurejesha mawasiliano na Waajiri wake wa zamani mitaa ya Jangwani.