Mchezaji Sadio Mane Aitanguliza Senegal Fainali AFCON......



Usiku wa kuamkia leo ulikuwa sio rahisi sana kwa Taifa la Senegal licha ya ushindi wa goli 3 kwa 1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa nusu fainali ya AFCON.

Kipindi cha kwanza kiliisha kila timu ikiwa haijaona lango la mwenzie lakini 45 za kipindi cha pili zilitumika vizuri na Sadio Mane ambaye alifunga goli moja na kutoa pasi ya goli lingine ambalo lilifungwa na Idrissa Gana Gueye na lingine likifungwa na Abou Diallo.

Bao la kufutia machozi la Burkina Faso lilifungwa na Toure dakika ya 82’. Burkina Faso michuano hii licha ya kutolewa walionyesha upinzani mkubwa na sasa wanasubiri kucheza mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu Jumamosi.

Senegal wamefika mara tatu fainali katika historia ya michuano hii, mara moja AFCON 2012 Aliou Cisse akiwa mchezaji na mara mbili akiwa kocha.

Leo ni kivumbi na jasho kwenye nusu fainali nyingine ambayo itawakutanisha wenyeji Cameron dhidi ya Mafarao wa Misri.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad