Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi ambaye ni Mchungaji wa kanisa la Zumaridi, kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa binadamu 149 wakiwemo watoto wenye umri kati ya miaka 4 hadi 17.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi amesema, polisi walipokea amri ya mahakama ya mwanzo Mkuyuni kumtafuta na kumkamata mzazi wa mtoto Samir Abbas aliyetakiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kwenda shule kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu ndipo polisi walipobaini mzazi huyo pamaoja na mtoto wake kuwepo nyumbani kwa mchungaji huyo anayejiita mfalme na baada ya kufika nyumbani hapo ndipo walipowakuta watu wengine 149 kati yao wakiwemo watoto 24.
Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi ambaye ni Mchungaji wa kanisa la Zumaridi
Katika tukio lingine kamanda Ng'anzi amesema jeshi la polisi limetekeleza maelekezo ya mwendesha mashtaka wa Serikali DPP ya kuwaachia watuhumiwa 39 wa makosa ya ugaidi ambao wamekidhi masharti ya dhamana.