Misri Kucheza na Senegal Katika Fainali AFCON....Wenyeji Cameroon Hawaamini



Timu ya taifa ya Misri ikisheherekea baada ya kuifunga Cameroon mabao 3-1 kwa njia ya penati na kutinga fainali ya Afcon.
Timu ya taifa ya Misri ikisheherekea baada ya kuifunga Cameroon mabao 3-1 kwa njia ya penati na kutinga fainali ya Afcon.
Timu ya taifa ya Misri Pharaos imeingia tena katka fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2021 baada ya kuwafunga wenyeji Cameroon-Indomitable Lions kwa penati 3-1 baada ya dakika 120 za sare ya 0-0.

Washambuliaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi na Vincent Aboubakar walikuwa chini ya ulinzi mkali wa Misri ukiongozwa na kiungo mkabaji Mohamed El Nany ambao walifanya kazi kubwa kuwazuia.

Naye golikipa nambari mbili wa Misri Mohamed Abou Gabal Ali maarufu kama Gabaski pia alifanya kazi ya ziada kuzuia michomo ya washambuliaji wa Cameroon.

Na hatimaye wakati wa penati kipa huyo amekuwa shujaa wa timu hiyo kwa mara nyingine tena kwa kudaka penati mbili za Cameroon.


Kwa upande mwingine washambuliaji wa Misri Mo Salah na Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan au maarufu Trezeguet walikuwa wakipeleka mashambulizi kadhaa langoni mwa Cameroon lakini kazi ya ziada ilifanywa na mabeki wa timu hiyo kuwazuia.

Naye kocha wa timu ya Misri atakosa mechi ya fainali ya timu yake baada ya kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje ya uwanja na pia katika hali isiyo ya kawaida msaidizi wake Wael Gomaa,naye alipachikwa kadi ya njano ikiwa ni ya pili kwa maana hiyo wote watakosa kuwapo katika benchi la ufundi katika mechi ya fainali siku ya jumapili.

Sasa fainali ya kihistoria inakutanisha mafahali wawili wachezaji soka mashuhuri wa timu ya soka ya Liverpool Mo Salah na Sadio Mane wakicheza katika timu tofauti. Mafarao wa Misri wanapambana na Lions of Teranga Senegal katika fainali siku ya jumapili.

Wakati wenyeji Cameroon watapambana na Burkinafaso katika kuwania nafasi ya tatu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad