Mjenzi daraja la JPM atumbukia ziwani




Mwanza. Mwendesha mitambo inayofanya kazi katika daraja la JPM Kigongo Busisi mkoani Mwanza, Twalib Abas (35) amefaiki baada ya kreini aliyokuwa akiendesha kutumbukia kwenye ziwa usiku baada ya baada ya kugonga ukingo wa daraja la muda.

 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kuopoa mwili wa marehemu leo Jumapili Februari 13, 2022 mchana.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amesema tukio hilo limetokea wakati opareta huyo akipita kwenye daraja hilo la muda kutokea katikati kuelekea nchi kavu akiwa katika kutekeleza majukumu yake.

Amewataka watumishi wanaofanya kazi katika daraja hilo kuwa makini wanapotekeleza majukumu yako Ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.


 
Kamanda wa Zimamoto na Uokaji Mkoa wa Mwanza, Ambene Mwakidele amesema wametumia saa mbilii kuopoa mwili wa Marehemu huyo uliokuwa umezama ndani ya ziwa Victoria.

Amesema kwa sasa wana kazi moja ya kuhakikisha wanakitoa chombo kilichozama ndani ya ziwa Victoria.

Kaka wa marehemu Mohamed Yasin amesema marehemu alikuwa mzoefu katika kazi hizo,kwamba amefanya katika maeneo mbalimbali ikiwamo barabara ya za juu za Mfugale Dar es Salaam.


Amesema mwili wa mdogo wake utazikwa nyumbani kwake Mkola Mwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad