Mkata Umeme Simba Asiye na Bahati kwa Mashabiki



Licha ya Klabu ya Simba kuanza vibaya kwenye michezo ya mzunguko wa kwanza wa NBC Premier League msimu huu lakini timu hii imeonekana kua imara sana kwenye eneo lao la kiungo ambalo kwa sasa linaongozwa na wachezaji wawili matata ambao ni Jonas Mkude na Sadio Kanoute.

Baada ya kiungo mkata umeme wa klabu ya Simba Sc Taddeo Lwanga kupata majeraha ya muda mrefu mwanzoni mwa msimu huu, mashabiki wa klabu ya Simba Sc alianza kupata hofu sana na ndipo benchi la ufundi la klabu hiyo walipofanya maamuzi ya kumuibua Mkude ambaye alikua benchi kwa muda mrefu kutokana na tabia zake za utovu wa nidhamu.

Wakati Simba wanaibuka na Mkude ambaye amezoeleka katika eneo la kiungo la klabu ya Simba Sc kwa miaka mingi iliyopita, klabu hii walikua tayari wameanza kumtumia Sadio Kanoute kutoka nchini Mali ambaye alianza kucheza soka katika ardhi ya Tanzania kwenye mchezo wa Simba Sc dhdi ya Tp Mazembe siku ya Simba Sc katika dimba la Benjamini Mkapa.

Kanoute alionyesha kiwango bora sana licha ya kwamba alikua na hofu ya kucheza soka ugenini kama ilivyo kwa wachezaji wote duniani. Umati wa mashabiki wa klabu ya Simba Sc ambao walifurika katika dimba la Benjamini Mkapa siku hiyo wakizidi kumuongeza hofu kiungo huyu ambaye sasa ameongia kwenye imani ya Pablo Franco.


 
Kanoute ni kiungo mwenye tabia ya kuzuia mashambulizi kutoka kwa wapinzani ambapo mara nyingi amekua anaonekana kucheza juu ya Inonga na Onyango ambao wanafunga safu ya ulinzi ya Simba Sc kupitia eneo la katikati la uwanja.

Kimo cha Kanoute ni faida kwake kuweza kucheza mipira ya juu, akili kubwa iliyopo kichwani kwake inatoa nafasi kwake kuweza kuzuia mashambulizi ya mipira ya chini.

Wewe kama mdau na shabiki wa soka nchini Tanzania utakua shahidi wa Kanoute juu ya uwezo wake mkubwa ndani ya NBC Premier League licha ya kwamba jina lake halina bahati ya kuimbwa sana na mashabiki wa klabu ya Simba Sc ambao wamekua na upofu mkubwa juu ya nyota huyu mpole akiwa uwanjani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad