Mlipuko Waripotiwa Kutokea Katika Bomba la Gasi Ukraine



Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv umekabiliwa na mashambulio makali ya Urusi, kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Ukraine imesema kuwa wanajeshi hao wa Urusi pia wanakabiliwa na upinzani mkubwa ikiwa pamoja na vikosi hivyo vya nchi hiyo kuzuia shambulio la Urusi karibu na mji wa Kharkiv ulio kaskazini, mashariki mwa Ukraine.

Ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy imesema kumetokea mlipuko kwenye bomba la gesi, kusini mwa mji mkuu wa Kiev mapema Jumapili ambapo Amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji huo mkuu wa hadi kesho Jumatatu.

Wakati huohuo Mataifa ya Magharibi yanapanga kuziondoa baadhi ya benk za Urusi kutoka kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa (SWIFT).

Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani Andrij Melnyk ameelezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka silaha nchini Ukraine naye Balozi Andrij Melnyk ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria.


Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR, limesema takriban watu 150,000 wamekimbia mapigano kutoka Ukraine na kuingia katika mataifa jirani.

Msemaji wa UNHCR, Shabia Mantoo, ameeleza kuwa idadi hiyo inaoongezeka kila dakika na shirika hilo la kuwashughulikia wakimbizi, linakadiria kuwa huenda takriban watu milioni 4 wa Ukraine wakaikimbia nchi hiyo iwapo hali itaendelea kuwa mbaya. Mantoo amesema watu wengi wanakimbilia katika nchi jirani za Poland, Moldova, Hungary, Romania na Slovakia na Belarus.

Nchi za Magharibi zinapanga kuzitoa benki fulani za Urusi kutoka kwenye mfumo wa benki wa SWIFT. Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema hatua hiyo itahakikisha kwamba benki zitasitisha ushirikiano na Urusi katika mfumo wa kimataifa ili kutatiza maswala ya kifedha ya Urusi kimataifa.


Ujerumani, Umoja Ulaya, Marekani na Uingereza zimetangaza vikwazo hivyo vipya dhidi ya Urusi ingawa awali Ujerumani ilipinga hatua hiyo ikisema inaweza pia kuudhuru uchumi wa dunia.

Kwa upande wake Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo Jumapili kwa mara ya nne ndani ya wiki moja. Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia watashiriki kwenye mkutano huo kwa njia ya video kujadili msaada zaidi kwa Ukraine na hatua zaidi za adhabu dhidi ya Urusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad