Mdhamini wa Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' amesema kilicho mpeleka kambini ni mapenzi yake dhidi ya Simba na amemua kuvua nguo lazima ayaoge, amekuja amekutana na viongozi wachezaji kwa ajili ya kuwapa hamasa.
Mo Dewji amesema wakati huu wapo katika kombe la Shirikisho Afrika lazima wajipange kwa sababu ni mashindano ya kweli ila bado wanakazi ngumu kwenye ligi na lazima kuwa na malengo makubwa.
"Ukweli kwanza kuwekeza ndani ya Simba ni hasara bado tunapambana sana kuifikisha Simba katika bajeti kubwa ya kujiendesha yenyewe, katika miaka minne nilikuwa kiongozi ila sasa hivi sina mamlaka yoyote," alisema Mo Dewji na kuongeza;
"Nipo pamoja sana na Mwenyekiti, Salim Abdalla 'Try Again', Bodi ya wakurugenzi pamoja na mashabiki kuendelea kuisaidia timu ili kuwa na bajeti kubwa kushindana na klabu kama Al Ahly,"
Mo Dewji alisema sawa wanahuzunika kwa nini Simba imekuwa kwenye klabu kumi bora Afrika kwa sababu wanashindana katika Ligi ya mabingwa ila bahati mbaya mwaka huu wametolewa.
"Unajua Simba ni klabu kubwa Afrika na tunatakiwa kuwa na muendelezo wa kucheza robo, nusu fainali mara kwa mara ya mashindano ya kimataifa lakini la pili Super Cup sina taarifa nalo ila viongozi wakubwa wa Simba walienda Misri katika mkutano na bado hawajanipa feedback yoyote.
"Naamini kwamba mafanikio ya Simba ni mashabiki na wiki hii tuna mechi ngumu na wakijitokeza watu 3,5000, Mungu atujalie hizo pointi tatu tutapata na nitakuwepo uwanjani, kwani bila ya mashabiki hakuna Simba wala Mo Dewji," alisema Mo Dewji.
Katika hatua nyingine Mo Dewji alisema amewapa motisha wachezaji na la pili waone ya Simba katika miaka minne wamefika hatua ya makundi na robo fainali.
"Kitu ambacho tunataka awamu hii ni kuvuka katika hatua ya robo fainali na kuweka historia kwani wachezaji nao wataingia kwenye historia ya Tanzania na ya Simba kitu ambacho tunataka tusonge mbele zaidi kwani hapo siku na watasema wameitumikia Simba tushinde ubingwa wa Afrika na kombe la Shirikisho Afrika," alisema Mo Dewji.