Morocco imemfanyia mazishi ya "Rayan", mvulana mwenye umri wa miaka mitano aliyefariki baada ya kunaswa kisimani kwa siku nne.
Rayan Oram alianguka chini kwenye kisima cha mita 32 (futi 104) tarehe 1 Februari, na hivyo kuzua juhudi kubwa za kumwokoa.
Mamia walikusanyika kisimani, huku juhudi za uokoaji zikivuta hisia za wanahabari kote ulimwenguni.
Mazishi yake yalifanyika mapema Jumatatu katika kijiji chake kaskazini mwa milima ya Rif ambapo mkasa huo ulitokea.
"Kimya cha kutisha kilikumba kijiji hicho asubuhi ya leo i," jamaa aliambia shirika la habari la AFP.
Wakati mvulana huyo hatimaye alipotolewa kutoka kisimani Jsiku ya umamosi jioni, uokoaji wake dhahiri ulipokelewa na shangwe kutoka kila sehemu.
Lakini hii iligeuka kuwa huzuni dakika chache baadaye wakati ilitangazwa kuwa uokoaji ulikuwa umechelewa, na Rayan alikuwa amekufa.
Ujumbe wa uokoaji ulikuwa ukitazamwa kote ulimwenguni - na mara baada ya kifo kutangazwa, jumbe za rambirambi zilimiminika.
Kwenye mitandao ya kijamii, ambapo alama ya reli #SaveRayan ilikuwa ikisambaa, watu walionyesha huruma na huzuni zao.
Mfalme wa Morocco Mohammed VI aliwaita wazazi wa mvulana huyo na kuwapa rambirambi zake nyingi.
Papa Francis, huku akielezea masikitiko yake, alisifu njia "nzuri" ambayo watu "walifanya kazi pamoja kuokoa mtoto".
Shabiki wa Misri akibeba picha ya Rayan katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika siku ya Jumapili
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha,
Shabiki wa Misri akibeba picha ya Rayan katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika siku ya Jumapili
Wachezaji na mashabiki katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili nchini Cameroon walikaa kimya kwa muda kumuenzi Rayan.
Baba ya Rayan, Khaled Aourram, alikuwa akitayarisha kisima hicho wakati mvulana huyo alipoanguka.
Mchanganyiko wa udongo wa mawe na mchanga kwenye shimo hilo ulilifanya kuwa hatari iwapo waokoaji wangechimba shimo jingine dogo la kisima cha maji.
Badala yake, tingatinga zilitumiwa kuchimba mtaro mkubwa karibu na kisima hicho.
Picha zinazoonesha urefu wa kisima hicho
Short presentational transparent line
Waokoaji walijaribu kupeleka oksijeni, chakula na maji kwa mvulana huyo, lakini haikujulikana ikiwa aliweza kuvitumia.
Picha za Alhamisi kutoka kwa kamera iliyoshushwa ndani ya kisima zilionyesha kuwa mvulana huyo alikuwa hai na anafahamu, lakini hakukuwa na sasisho za hali yake baada ya hapo.
"Tunamshukuru Mtukufu Mfalme, mamlaka na wale wote ambao wametusaidia," babake alisema Jumamosi jioni. "Mungu asifiwe, warehemu wafu."