Klabu ya Simba imethibitisha kutopokea barua ya maelezo kutoka kwa mchezaji wao Bernald Morrison ambaye wamemsimamisha kwa makosa ya utovu wa nidhamu, Februari 4, 2022. ambapo klabu ya Simba ilitoa taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa Ofisa wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema klabu bado haijapokea maelezo kutoka kwa mchezaji wao Bernard Morrison. Mchezaji huyo anapaswa kuandika barua ya maelezo kwenda kwa mtendaji mkuu