Msemaji wa Simba "VAR Sio Tatizo la Msingi la Mpira Wetu Bongo, Tatizo ni Sehemu ya Kuchezea"


“Nimeona mjadala wa VAR 👏👏 ni wazo zuri naamini nia ni kuufanya mpira wa nchi hii uendelee kuwa bora zaidi.

Lakin kwangu VAR sio tatizo la msingi la mpira wetu

Tatizo la msingi la mpira wetu ni sehemu ya kuchezea ( PITCH)

Tuna pitch mbovu sana nchi hii ukitoa Taifa, Azam Complex na Kaitaba, viwanja vingi vilivyosalia ni changamoto

Mpaka leo viwanja vyetu vinapakwa chokaa kabla ya mechi na baada ya muda chokaa inafutika uwanja unakua hauna mistari

Mvua zikinyesha kidogo tuu mpira hauchezeki

Mechi nyingi zinachezwa kwa kulazimishwa mfano mechi ya Mbeya City Vs Ruvu Shooting haikupaswa kuchezwa pale Sokoine

Ushauri wangu kabla ya ku invest kwenye VAR tungejikita kuboresha viwanja

Europe walianza kuboresha viwanja ndo wakaja kwenye VAR

Na kabla ya kufika kwenye VAR mamlaka husika waendelee kuboresha viwango vya waamuzi wetu wapate seminar za kutosha na wapate mechi kubwa za Afrika ili kuongeza uzoefu na kujiamini kwao

Tukishamaliza kuwekeza kwenye Pitch ndo tutakuja kwenye VAR,” ✍🏽 Msemaji wa Simba Sc, @ahmedally_

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad