Msuva Afunguka Kuhusu Wapi Atacheza Msimu Ujao




KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa watulivu na muda ukifika ndiyo ataweka wazi kila kitu kuhusu anachopitia kwa sasa kwenye soka.

Msuva alifunguka kuwa akili yake kwa sasa anaielekeza kwenye kufanya mazoezi zaidi ili kuendelea kuwa fiti na ndiyo maana amekuwa mgumu kuzungumza na vyombo vya habari kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Msuva alisema yeye ndiye anajua kila kitu kuhusu wapi atacheza msimu ujao na nini kinaendelea juu ya masuala yake ya kimkataba na klabu ya Wydad Casablanca na wakati wa kuweka wazi ukifika atasema na watu wanapaswa kuwa watulivu.

“Watanzania watulie tu kwa sasa, mimi nitasema muda ukifika nini kinaendelea kwangu, kwa sasa akili yangu naelekeza zaidi kwenye kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa fiti zaidi,” alisema Msuva.

Msuva yupo nchini takribani miezi miwili sasa, ikidaiwa ameondoka Wydad Casablanca kwa sasa, anahitaji kulipwa maslahi yake ya kimkataba ikiwemo fedha za usajili, huku taarifa zikiibuka kuwa TP Mazembe wapo wanawinda saini yake pia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad