Mtanzania mwenye asili ya Kimasai, Kili Paul Aliyepata Umaarufu Mkubwa India Aitwa Ubalozini


Mtanzania mwenye asili ya Kimasai, Kili Paul akiwa kwenye ofisi za high commission ya India nchini Tanzania

Kili Paul na dada yake Neema Paul wameweza kuiteka haraka mitandao ya kijamii bila skendo au mambo ya ajabu ajabu, wasanii hao wamejipatia umaarufu kwa kuimba nyimbo za filami za kihindi wakati huo huo wakiutangaza utamaduni wa Kimasai

Kili tayari alijizolea followers takribani milioni mbili TikTok na baadaye alipofungua Instagram kwasasa ana followers zaidi ya milioni 2.2 ndani ya muda mfupi tu huku asilimia karibia 90% ya followers wake wakiwa ni wahindi wakiwemo mastaa wa filamu kama Ayushmann Khurana, Richa Chadha etc mastaa wengine wakubwa wakiwemo Sidhath Malhotra na Kiara Advan hawakusita kumpongeza kwa anachokifanya

Hivi juzi kati BBC World News walifanya pia kuangazia anachokifanya msanii huyo na dada yake

Kili anazungumza kiingereza vizuri, na video zao mara nyingi wanaarekodi kwa simu wakiwa kijijini, Kila ambaye kwasasa amegeuka celebrity hasa kwa India sababu ya kila siku media za huko kuandika kuhusu yeye

Wakihojiwa na gazeti la Hindustani Times Kili Paul amesema kuwa anapenda filamu za kihindi muda mrefu na anavutiwa zaidi na filamu za action ambapo mastaa anaowakubali zaidi ni Hrithik Roshan, Salman Khan na Tiger Shroff, amesema kwa upande wa Neema Paul yeye anavutiwa zaidi na mwigizaji maarufu Madhuri Dixti

Kili na Neema walianza kuimba nyimbo za Kiswahili hata hivyo hawakupata support nzuri, walipoanza kuimba kihindi ghafla wakapata attention kubwa hasa baada ya vyombo vya habari vya huko India kuripoti kuhusu wao kisha mastaa wa kihindi nao kuwapa airtime

Posts za wawili hao kila siku zinajaa LIKES na comments nyingi hasa kutoka mwa mashabiki wao wa Kihindi, Kili pia akihojiwa amesema wahindi wanawaonesha support kubwa hata comments zao zinawahamasisha wasonge mbele zaidi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad