Mtia Nia Uspika: Nitawanunulia Wabunge Magari Mazuri, Nitaongeza Posho



Mgombea wa Kiti cha Spika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kunje Ngombale Mwiru kutoka chama cha Sauti ya Umma (SAU) amewaeleza wabunge wakati akiomba kura kuwa akipata ridhaa ya kuwa spika hato kwenda kuongoza bunge la Uganda.

Awali Mbunge wa Viti Maalum, Jackline Ngonyani (CCM) alitaka mtia nia huyo athibitishe kuwa atakuwa ni kiongozi mwenye msimamo na asiyeyumbishwa kwa kuwa bunge linahitaji kuongwazwa na mtu mahili asiye hitaji kuyumbishwa yubishwa.

Ngonyani alidai kuwa mtia nia ameonesha uzoefu wa kuhama hama vyama. “Ameonesha hapa ana zaidi ya vyama vitano, amehama hama na hii inaonesha kwamba hana msimamo katika kujiunga na vyama lakini katika kusimama kwenye vyama hivyo.”

Hata hivyo mwenyekiti wa Uchaguzi, William Lukuvi aliomuomba Mwiru kutojibu kwa kuwa sio swali na kuwa katiba ya nchi inatoa haki ya mtu kuwa na uchaguzi wa chama cha kisiasa.


 
Ngombale Mwiru akijinadi aameahidi kupunguza idadi ya vikao vya bunge na kuongeza posho zao. Aidha, ameahidi kutoa magari imara kwa wabunge na yasiyo ya mikopo ili wafike mjimboni bila usumbufu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad