IDRISSA Mkenge (16), mkazi wa Magomeni, mkoani Dar es Salaam, ambaye alikuwa anatafutwa na wazazi wake baada ya kutoripoti shuleni tangu alipoaga nyumbani Januari 15, mwaka huu, amepatikana jana kwenye mazingira ya kutatanisha, eneo la Upanga.
IDRISSA Mkenge akiwa na baba yake Haji Mkenge.
Juzi, baba mzazi wa mtoto huyo, Haji Mkenge, alifika ofisi za Nipashe, Mikocheni kutoa taarifa ya kupotea kwa mwanae, aliyekuwa akisafiri kutoa Dar es Salaam kuelekea shuleni Kibaha mkoani Pwani anaposoma katika Shule ya Sekondari Sambo baada ya kumaliza likizo ya mwisho wa mwaka.
Akizungumza leo na Nipashe, Mkenge, amesema kwa maelezo ya mwanae baada ya kupatikana ni kwamba akiwa safarini alishuka eneo Mbezi Mwisho na kula chakula lakini baada ya hapo hakumbuki kilichoendelea tangu apate mlo huo.
"Amepatikana jana Februari 02 akiwa kama amechanganyikiwa waliomuona akiwa, anaombaomba.Aliyemuona ni mtoto ambaye tuliwahi kuishi nae Kinondoni ila yeye kwa sasa anaishi Upanga alimkuta eneo hilo.
"Usiku nikawaambia baadhi ya wenzangu watembelee eneo ambalo mtoto alionekana, asubuhi wakamtafuta, wakamkuta eneo la Upanga-Muhimbili, akiwa amevaa kaptula, na t-shirt ambazo si nguo alizoondoka nazo.