Mtoto mwenye umri wa miaka 13 anayejulikana kwa jina la Faidhati Ibrahim ameuawa na binadamu yake aliyefahamika kwa jina la Shomari Malima kwa kukatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo shingoni na kichwani.
Tukio hilo limetokea Jana Februari 15, 2022 majira ya saa 11 jioni katika mtaa wa Tambukareli kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro ambapo mtuhumiwa alifika katika nyumba ya familia hiyo na baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa peke yake alianza kutekeleza unyama huo.
Faidhati Ibrahim alikuwa mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mwenge iliyopo kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Juma Muitano amekiri kutokea kwa tukio hilo.