Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.
Tukio hilo linadaiwa kutokea jana Alhamisi Februari 3,2022 majira saa 12 jioni baada ya marehemu akiwa na mtoto mchanga wa miezi 4 kumkabidhi mtoto huyo kwa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wagenina baada ya masaa 4 aligundulika akiwa amefariki duhia baada ya kukutwa akiwa amejining’iniza kwa kamba iliyodaiwa kufungwa juu ya dali chooni.
Mhudumu wa nyumba hiyo ya wageni iliyopo Katoro mjini Monica Paulo amesema mke wa mwajiri wake, alifika kwenye nyumba hiyo majira ya saa 8 mchana na kumtaka amsaidie kubeba mtoto akapumzike akidai hajisikii vizuri kiafya.
Monica ameeleza kuwa marehemu aligundulika baada ya Mteja mmoja kufika na kuomba huduma huduma ya choo na akakuta mtu kajinyonga chooni.
Kiongozi wa eneo hilo Stephano Bandola amekiri kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa chanzo cha tukio hilo kinaweza kuwa ni migogoro ya kufamilia.
Imeelezwa kuwa wakati tukio hilo kukitokea,mume wa marehemu alikuwa safarini.