Mapya yaibuka ! Mwanaume wa miaka 54 amwagia tindikali(acid) mpenzi wake ambaye ni binti wa miaka 18 pamoja na mama mzazi wa binti husika
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Ghana, mwanaume huyo mfanyabiashara alivujisha video ya uchi ya binti huyo kitu ambacho kilipelekea mama mzazi kuongozana na binti yake wakaenda kumripoti kwenye vyombo vya sheria ambapo mwanaume huyo alitakiwa kutoa faini kwa kufanya kosa la kusambaza picha za utupu na pia kutozwa faini kwa kumchafua binti huyo kwa kuvujisha video
Haijajulikana mara moja sababu ya mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 54 kuvujisha video ya ngono ya mpenzi wake huyo mwenye miaka 18, lakini walipotoka kwenye vyombo vya sheria mwanaume huyo akawavizia tena na kuwamwagia tindikali binti na mama yake na kupelekea kuwahishwa hospitalini