Mwenyekiti CCM Mara alipua mafisadi



MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye amewalipua watendaji wa vijiji na madiwani mkoani Mara akidai kuwa ni wala rushwa, wabadhirifu, wanatumia vibaya madaraka na yupo tayari kuwataja.

Kaboye aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye sherehe za uwekaji jiwe la msingi, ujenzi wa chujio la maji katika mradi wa maji Bunda, mkoani Mara.

Alimuahidi Rais Samia kuwa atampelekea majina ya watu wote wanaopokea rushwa wakiwemo madiwani wanaochukua zabuni za halmashauri kinyume cha sheria.

“Mkoa wa Mara wanaopokea rushwa nitakuletea majina yao hata leo hii (jana) na wengine wako serikalini. Nakuambia ukweli wengine wanaweza kuniwekea sumu kwenye maji ili nife na wengine wameniambia siwezi kuwataja kwa kuwa mwaka huu kuna uchaguzi, mimi namtegemea Mungu tu,” alisema Kaboye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad